Alitoa pongezi hizo baada ya kushinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo uliofanyika Jumapili, taarifa ilisema.
“Kwa kuzingatia muelekeo wa matokeo ya uchaguzi wa rais na kusubiri tangazo rasmi, nampongeza rais Bassirou Diomaye Diakhar Faye kwa ushindi wake wa duru ya kwanza” alisema Ba katika taafa hiyo.
Uchaguzi huo umekuja baada ya hatua ya awali ya rais anayeondoka madarakani Macky Sall kutaka kuahirisha uchaguzi kuzua hofu ya kuwa anataka kujaribu kushikilia madaraka.
Katika uchaguzi huo, maelfu ya Wasenegali walijitokeza katika maeneo mbalimbali nchini walisubiri kwa utulivu kupiga kura zao, Abdoulaye Sylla, president rais wa Tume ya Uchaguzi amesema idadi kubwa ya watu walijitokeza.
Waangaliazi kutoka mashirika mengi walikuwepo, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Ulaya, ambao ulituma waangaliazi 100 katika meneo mbalimbali nchini.
Faye mpinzani wa viongozi walioko madarakani ameahidi kurejesha “mamlaka ya nchi” kupambana na ufisadi na kuleta uwiano wa kiuchumi.
Baadhi ya taarifa ya habari hii inatoka mashirika ya habari ya Reuters na AFP