Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 05:28

Rais wa Senegal Macky Sall ameiambia serikali yake kutunga sheria ya msamaha

 Rais wa Senegal Macky Sall akitoka baada ya kukutana na rais wa France June 23, 2023.Picha na Ludovic MARIN/ AFP
Rais wa Senegal Macky Sall akitoka baada ya kukutana na rais wa France June 23, 2023.Picha na Ludovic MARIN/ AFP

Rais wa Senegal Macky Sall ameiambia serikali yake kutunga sheria ya msamaha punde tu itakapochapishwa rasmi, huku kukiwa na matumaini kwamba mgombea mkuu wa upinzani aliyefungwa jela anaweza kuachiliwa huru kabla ya uchaguzi wa urais ndani ya siku 10.

Katika jitihada za kumaliza machafuko ya wiki kadhaa baada ya kuahirisha kura ya urais ya Februari 25, Sall alipendekeza muswada wa kutoa msamaha kwa vitendo vilivyofanywa kuhusiana na maandamano ya kisiasa tangu mwaka 2021.

Sheria hiyo iliyopitishwa na wabunge wiki jana, inatarajiwa kuchapishwa mara moja lakini hakuna taarifa rasmi wakati gani inaweza kutokea.

Mgombea wa upinzani gerezani, Bassirou Diomaye Faye, na kiongozi wa muungano wake anayezuiliwa, Ousmane Sonko, wanaweza kuwa wanufaika wakuu.

Forum

XS
SM
MD
LG