Viongozi wa Senegal wanaoupinga utawala wa nchi wameibuka na nguvu kutokana na mapambano ya miaka mitatu dhidi ya serikali ya Rais Macky Sall na mahakama, baada ya kuachiliwa kutoka gerezani kabla ya uchaguzi wa mwezi huu, wachambuzi wanasema.
Kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko na mgombea wake namba mbili wa urais, Bassirou Diomaye Faye sasa wanaweza kutumia kasi mpya kwa ajili ya uchaguzi wa Machi 24 baada ya wiki kadhaa za mgogoro.
Waliachiwa huru siku ya Alhamisi chini ya sheria ya msamaha iliyopendekezwa na Sall katika juhudi za kuzima wiki kadhaa za ghasia zilizopelekea ghasia mbaya sana kwa kuchochewa na na Sall kuahirisha uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 25.
Forum