Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 01:18

Mwanamke wa kwanza kuwania urais wa Senegal Jumapili


Mgombea urais mwanamke wa Senegal, Anta Babacar Ngom, akifanya kampeni zake mjini Dakar, Machi 11, 2024.
Mgombea urais mwanamke wa Senegal, Anta Babacar Ngom, akifanya kampeni zake mjini Dakar, Machi 11, 2024.

Mwanamke wa kwanza kugombea urais kwenye uchaguzi wa Jumapili wa Senegal, huenda asipate ushindi, lakini wanaharakati wanasema kwamba kuwepo kwake kunasaidia kampeni ya muda mrefu ya kufikia usawa wa kijinsia kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi.

Anta Babacar Ngom, mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 40, ni sauti ya wanawake na vijana, makundi ambayo yameathiriwa vibaya sana na hali ngumu ya uchumi, ukosefu wa ajira, na kupanda kwa bei za bidhaa.

Kwenye kampeni zake, Ngom, amekuwa akiahidi kutengeneza mamilioni ya ajira, pamoja na benki ya wanawake, kwa lengo la kuwainua kiuchumi. Katika mahojiano ya hivi karibuni na shirika la habari la AP, Ngom alisema kwamba “ Taifa letu lina uwezo mkubwa sana, rasilimali za asili ziko na zinaweza kuendelezwa.”

Ngom ni mwanamke wa kwanza kuwania urais nchini humo baada ya zaidi ya muongo mmoja, ishara ya kasi ndogo ya mabadiliko, kulingana na wanaharakati, ambao wanasema kuwa vijana wameanza kubadili dhana za kitamaduni kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii.

Forum

XS
SM
MD
LG