Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken alikutana na Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador siku ya Jumatano katika mashauriano ya faragha.
Kwenye mtandao wa kijamii, Lopez Obrador alisifu kile alichokielezea kama makubaliano muhimu lakini hakutoa maelezo.
Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka ya Marekani mapema mwezi huu ilifunga kwa muda vivuko viwili muhimu vya reli kati ya Texas na Mexico, na kufunga vivuko vingine, ili kukabiliana na msongamano mkubwa wa wahamiaji.
Waziri wa mambo ya nje Alicia Barena alisema Mexico ilitaka vivuko hivyo vifunguliwe tena.
Lopez Obrador wiki iliyopita aliihakikishia Marekani kwamba Mexico itasaidia kupunguza shinikizo la wahamaji.
Mapema Jumatano, alisema Bunge la Marekani linapaswa kuwekeza kwa watu maskini huko Amerika Kusini na Caribbean badala ya kufikiri juu ya kujenga ukuta.
Rekodi ya idadi ya watu wanaokimbia uhalifu, umaskini, na migogoro na kufika kwenye mpaka wa Marekani, ni suala muhimu kabla ya uchaguzi wa rais wa Novemba.
Rais Joe Biden anataka Mexico imsaidie kupunguza idadi hiyo, kabla ya azma yake ya kuchaguliwa tena.