Sheria hiyo ilitungwa mwaka 2015 kwa uratibu wa EU na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa za kulevya na uhalifu.
Wakati huo, Ulaya ilikuwa ikikabiliwa na mzozo wa wahamiaji, ambapo zaidi ya watu milioni moja waliingia barani humo kutoka Uturuki na Afrika Kaskazini.
Kama sehemu ya makubaliano ya 2015, Umoja wa Ulaya uliahidi msaada wa zaidi ya dola bilioni 5 ili kuleta utulivu wa uchumi na serikali katika eneo la Sahel ili kuzuia misafara ya wahamiaji.
“Miradi ilikuwa na malengo, ikiwa pamoja na kupambana na uhamiaji haramu, kuboresha miundombinu ya umma, kuboresha uwezo wa mpaka lakini pia kusaidia watu waliokimbia makazi yao,” alielezea Alia Fakhry, mtaalam wa sera za uhamiaji wa EU.
Forum