Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:32

Umoja wa Ulaya wafikia makubaliano kushirikiana gharama na majukumu ya kuwapokea wahamiaji


Bunge la Umoja wa Ulaya.
Bunge la Umoja wa Ulaya.

Umoja wa Ulaya umefikia makubaliano mapema Jumatano kuhusu kanuni mpya zilizowekwa kwa ajili ya kushirikiana gharama na majukumu ya kuwapokea wahamiaji kwa usawa zaidi na kudhibiti idadi ya watu wanaokuja.

Wawakilishi wa Bunge la Umoja wa Ulaya na serikali za EU wamefikia makubaliano baada ya mazungumzo ya usiku kucha kuhusu sheria za EU kwa pamoja zinazoitwa Mkataba Mpya wa Wahamiaji na Wanaoomba Hifadhi ambao utaanza kutumika mwakani.

Sheria hizo zinahusisha kuwatathmini wahamiaji wasiokuwa wa kawaida wanapowasili katika Umoja wa Ulaya, taratibu za kushughulikia maombi ya waomba hifadhi hao, kanuni zitakazoamua nchi ipi ya EU ina jukumu la kushughulikia maombi na njia za kukabiliana na migogoro.

Kuwasili kwa wahamiaji katika Umoja wa Ulaya umepungua kutoka idadi ya juu ya 2015 kwa zaidi ya milioni 1, lakini imekwenda juu kutoka idadi ya chini ya 2020 kufikia 255,000 katika mwaka huu hadi Novemba, huku zaidi ya nusu yao wakivuka Bahari ya Mediterranean kutoka Afrika kuja Italia au Malta.

Juhudi za nyuma kuweza kushirikiana majukumu ya kuwapokea wahamiaji zilianzishwa kwa sababu nchini wanachama wa mashariki wa EU hasa walikuwa hawakuwa tayari kuwapokea watu waliokuwa waliwasili Ugiriki, Italia na nchi nyingine.

Chini ya mfumo mpya, nchi hizo ambazo haziko mpakani zitakuwa na hiari kati ya kuwapokea wakimbizi au kulipa katika mfuko wa EU.

Mfumo wa kuwachunguza unaotarajiwa kutumika utatafuta kutofautisha wale wanaohitaji ulinzi wa kimataifa na wale ambao hawahitaji.

Watu ambao maombi yao ya hifadhi yana nafasi finyu ya kufanikiwa, kama wale kutoka India, Tunisia au Uturuki, wanaweza kuzuiliwa kuingia Umoja wa Ulaya na kukamatwa mpakani, kama ilivyo kwa watu wanaoonekana wanaweza kuwa tishio kwa usalama.

Vikundi vya haki za wakimbizi vimesema hii litafanya kuanzishwa kile kinachoonekana kuwa ni kambi za magereza katika mipaka ya EU.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG