Taarifa hii ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa kikundi hicho iliyotolewa Jumatatu, akiongezea kuwa matamshi ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kuhusu NATO ‘kwa hakika’ yatakuwa kwenye ajenda.
Mwenyekiti wa MSC Christoph Heusgen, balozi wa zamani wa Ujerumani kwa Marekani, aliwaambia waandishi wa habari mjini Berlin, wanadiplomasia wa juu wa Marekani, Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italy na Japan watakutana na pia kujadili matamshi ya Trump ambaye alisema hatawalinda wanachama wa NATIO kutokana na mashambulizi yajayo ya Russia kama mchango wa nchi hiyo kwa ushirika wa ulinzi utakuwa unalegalega.
Wakati wa mkutano wa kisiasa Jumamosi huko South Carolina, Trump alilalamika kuhusu kile alichokiita “kushindwa’ kulipa ada zao kwa baadhi ya nchi wanachama wa NATO na alikumbushia kile alichosema mawasiliano ya zamani na mkuu wa ‘nchi moja kubwa’ kuhusu shambulizi lililofanywa na Russia kwa nchi kama hizo.