Waziri wa afya wa taifa hilo Rajitha Senaratne amesema Jumatatu kundi la National Thowfeed Jamaath wanahusika na mashambulizi hayo.
Ameongeza kuwa, “bila ya mtandao wa kimataifa mashambulizi haya yasingeweza kufanikiwa.”
Senaratne amesema kuwa mashambulizi hayo katika maeneo sita – makanisa matatu na hoteli tatu – yalitekelezwa na watu saba waliojitoa muhanga kwa mabomu. Wote waliojitoa muhanga ni raia wa Sri Lanka, Senaratne amesema.
Shirika la habari la AP linaripoti kuwa washukiwa 24 tayari wamekamtwa kutokana na matukio hayo. Mapema Jumatatu amri ya kutotoka nje imetangazwa kuanzia saa mbili za usiku hadi saa kumi za asubuh
Gari moja lililipuka Jumatatu karibu na kanisa mojawapo ambapo mlipuko ulitokea Jumapili. Polisi walijaribu kulitegua mabomu yaliyokuwa ndani ya gari, laikini mabomu yaliripuka. Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
Rais wa Sri Lanka Maithripala Sirisena atatangaza hali ya hatari ya kitaifa kuanzia saa sita usiku Jumatatu. Vyombo vya habari vya ofisi ya Rais vimesema hatua hiyo ya dharura itatumika tu kupambana na ugaidi na haitazuia uhuru wa kujielezea.
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa washukiwa 24 wamekamatwa kutokana na milipuko hiyo.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.