Marekani yaomboleza kifo cha Jimmy Carter, ibada ya kumuaga yafanyika Washington

  • VOA News

Rais wa Marekani Joe Biden ambaye amezungumzia wasifu wa Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter katika Kanisa Kuu la Washington, DC, Januari 9, 2025. (Photo by Mandel NGAN / AFP)

Leo ni siku ya kitaifa ya maombolezo hapa Marekani kwa kifo cha rais wa zamani wa taifa hili Jimmy Carter, huku serikali ikiwa imefungwa na maafisa wajuu wamekusanyika katika Kanisa Kuu la Washington maarufu kama Washington National Cathedral kwa ajili ya mazishi ya kitaifa kwa rais wa 39.

Carter, ambaye alifariki wiki iliyopita akiwa na miaka 100 ambaye ni rais mzee wa zamani, mara nyingi hakujihusisha sana na taratibu za kisiasa za utawala wa Washington, lakini warithi wake wote watano walio hai marais – Bill Clinton, George W. Bush, Barack Obama, Donald Trump na Joe Biden walikuwepo kuhudhuria mazishi yake, huku Biden akizungumzia wasifu wa Carter.
Waombolezaji kwa upande wa umma walitoa heshima zao za mwisho kwa Carter ambaye jeneza lake lilifunikwa na bendera ya taifa, na kuwekwa kwenye ukumbi wa Bunge tangu Jumanne.
Baada ya mazishi, mwili wa Carter utasafirishwa nyumbani kwake katika jimbo la kusini la Georgia, ambako atazikwa katika shamba la familia karibu na Rosalynn Carter, mke wake kwa miaka 77 ambaye alifariki mwishoni mwa mwaka 2023.

Mjukuu Jason Carter katika ibada ya mazishi ya Rais wa zamani Jimmy Carter mjini Washington katika Kanisa Kuu, Jan. 9, 2025.

Heshima kwa Carter zilitolewa kwa wiki nzima, huku wengi wakimuelezea hivi sasa alivyoingia madarakani tangu mwanzo akiwa mnyenyekevu kama mkulima wa karanga na kuwa rais wa Marekani tangu 1977 mpaka 1981 wakati wa misukosuko nchini Marekani ilipokuwa inatoka kwenye kashfa ya kisiasa ya Watergate na kushindwa kwa jeshi katika vita vya Vietnam.
Carter Mdemocrat, alisimamia mashauriano ya mikataba ya Camp David, mkataba wa amani kati ya Misri na Israel, alishindwa kuchaguliwa tena mwaka 1980 na Mrepublican Ronald Reagan, lakini baadaye aliibuka katika maisha ya urais na kujishughulisha na masuala ya kibinadamu. Alipewa tuzo ya Nobeli ya Amani mwaka 2002 kwa juhudi zake ndefu kusimamia mashariano ya kupatikana kwa masuluhisho ya amani kwa mizozo mbali mbali duniani.
Mbali na Bide, mjukuu wa Carter, Jason Carter, na Stuart Eizenstat rafiki wa muda mrefu na mshauri wa masuala ya ndani katika White House wakati wa enzi ya Carter nao pia walipata fursa ya kumzungumzia rais wa zamani. Rais wa zamani alimshinda Mrepublican Rais Gerald Ford katika uchaguzi wa mwaka 1976, lakini baadaye walikuwa marafiki wakubwa.
Maelezo ya Ford na moja ya makamu rais wa Carter, Walter Mondale, yaliandikwa kabla ya vifo vyao, yatasomwa na watoto wao wa kiume, Steven Ford and Ted Mondale. Andrew Young, kiongozi wa haki za kiraia ambaye alihudumu wakati wa utawala wa Carter kama balozi kwenye Umoja wa mataifa, atatoa hotuba. Msanii wa Pop Garth Brooks na Trisha Yearwood wataimba wimbo wa John Lennon wa Imagine.

Amy Carter (aliyevaa miwani akiwa katikati) akiwa na wanafamilia akishuhudia mwili wa baba yake, Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter, wakati wakiondoka kutoka Bunge la Marekani kuelekea kwenye ibada ya mazishi huko katika Kanisa Kuu, Washington, Jan. 9, 2025.

Waombolezaji wa umma walitoa heshima zao kwa Carter baada ya kupata kwenye jeneza lake huko Capitol. David Smith, profesa katika shule ya Carter kwa Amani na Masuluhisho ya Mzozo katika Chuo Kikuu cha George Mason, amesema rais wa zamani kwa hakika amechangia katika kazi yake. Ameiambia VOA kuwa amefika Capitol kutoa heshima kwa mtu huyo na pia kuheshimu kazi za Carter.
“Alikuwa na mchango kwa watu wengi sana,” amesema. “Kazi yake ya kusukuma mbele walio wachache, uteuzi wa wanawake katika mahakama, kulinda mazingira yetu, kutetea haki za binadamu – mambo yote hayo ni muhimu sana kwangu mimi.”
“He had such an impact on so many people,” he said. “His work on katika ukumbi wa Capitol – ambako ni kiasi cha Wamarekani 50 tu wametambuliwa na kupewa heshima ya miili kuwekwa hapo tangu mwaka 1852 – kiongozi wa walio wengi katika Seneti John Thune, katika sala ya Jumanne jioni, alimuelezea Carter kuwa: “Mwanajeshi wa zamani wa Navy, mkulima wa karanga. Gavana wa Georgia. Na rais wa Marekani. Mwalimu wa Ibada ya watoto Jumapili. Mshinto wa tuzo ya Nobeli. Mtetezi wa amani na haki za binadamu. Kwanza kabisa, mtumishi muaminifu kwa muumba wake na wenzake.”
Makamu Rais Kamala Harris – ambaye siku ya Jumatatu huko Bungeni alirasmisha ushindi wa Trump kwa uchaguzi wa Novemba – alisisitiza sera za Carter.

Kutoka kushoto kwenda kulia, mstari wa kwanza, Rais Joe Biden, Mkewe Jill Biden, Makamu wa Rais Kamala Harris, Mume wa Makamu wa Rais Doug Emhoff, mstari wa pili, Rais wa zamani George W. Bush, mkewe Laura Bush, Rais wa zamani Barack Obama, Rais-mteule Donald Trump.

“Alikuwa rais wa kwanza wa Marekani kuwa na sera ya kina kwa nishati, ikiwa ni pamoja na baadhi ya uungaji mkono wa kwanza kwa nishati safi,” amesema Jumanne. “Pia alipitisha dazeni ya sheria kadhaa kuba kuhusu ulinzi wa mazingira. Na pia aliongeza mara mbili ukubwa wa hifadhi za taia Marekani.”
Carter alifariki Dese,mba 29 baada ya karibu miaka mwili kukaa chini ya huduma ya hospice nyumbani kwake huko Plains, Georgia. Tangu wakati huo, safari yake ya mwisho imeuchukua mwili wake katika Barabara nyembamba za mjini kwake, hadi kwenye mitaa mikubwa ya Atlanta, katika jengo la bunge jimboni hapo, na kupata kwenya anga hadi Washington iliyokumbwa na theluji, kwa ajili ya mazishi ya kitaifa.
Katika jengo la Bunge la Marekani, wabunge wameiambia jinsi Carter alivyokuwa kwao. Mbunge Alma Adams, Mdemocrat kutoka North Carolina, amesema Carter alikuwa ‘muadilifu wa kweli.” “Alifundisha masomo watoto kanisani kila Jumapili—nilifanya hivyo pia!” alisema akitabasamu. “Lakini nadhani kwa kweli aliwajali watu wote. Alikuwa rais wa watu.”
Mwakilishi Mrepublican wa South Carolina Ralph Norman ameiambai VOA kuwa wakati hakuwa kisiasa upande wa Carter, “Rais Carter alikuwa mtu mzuri. Rais Carter alikuwa mtu ambaye aliihudumia nchi yake. Aliipenda Marekani. Sikukubaliana na sera zake zote, lakini huwezi kukubali au kutokubali uzalendo wake, huwezi kukubaliana. Aliipenda nchi yake.”
Mwishoni mwa mwezi Desemba, baada ya kupata habari za kifo cha Carter, Biden alisema, “Sisi hatutamuona mtu kama yeye tena. Mnajua tunaweza kufanya vizuri ili tujaribu kidogo kuwa kama Jimmy Carter.”