Marekani kukabiliwa na wimbi la habari feki upya likitia ila matokeo ya uchaguzi

FILE PHOTO: John Kirby

Watengenezaji mashine za kupigia kura  huenda watalengwa na wimbi jipya la upotoshaji habari linalokusudia kutia ila matokeo ya uchaguzi wakati wapiga kura wa Marekani wakielekea katika vitu vya kupiga kura Jumanne.

Maafisa wa Marekani wakiwemo wale wa shirika linaloongoza kusimamia usalama wa uchaguzi, Shirika la Usalama wa Mitandao na Miundombinu ya Usalama (CISA), wamekuwa wakizuia madai ya uongo yanayopigiwa debe, wakieleza mengi kati ya hayo ujumbe wao unafanana, madai yaliyodhihiri kutoka uchaguzi wa urais wa 2020.

Mpiga kura akiweka kura yake katika uchaguzi wa katikati ya muhula 2022 huko Chapel Hill, North Carolina, Nov. 5, 2022.

Ujumbe huo pia umeelezwa na White House.

“Tunaamini kuwa Wamarekani wanaweza na wanatakiwa kwenda katika vituo vya kupiga kura na kujihisi wako salama na kwamba kila kitu kinafanyika kuhakikisha kuwa uchaguzi huu ni huru na haki na salama,” John Kirby, mratibu wa Baraza la Usalama la Taifa kwa ajili ya mawasiliano ya kimkakati,” aliwaambia waandishi wa habari Ijumaa iliyopita.

Wakazi wa eneo la Columbus, Ohio, Nov. 5, 2022, wakisubiri kupiga kura zao katika uchaguzi wa katikati ya muhula 2022.

Lakini utafiti mpya kutoka kampuni ya usalama wa mitandaoni Recorded Future imegundua kuwa kuna , viashiria kuwa juhudi za kueneza habari potofu zikilenga mashine za kupigia kura na mifumo ya kupiga kura kuna uwezekano zikaongezeka siku ya uchaguzi na siku kadhaa baada ya uchaguzi, japokuwa juhudi hizo siyo rahisi kulingana na shinikizo lililokuwepo miaka miwili ilyopita.