Taarifa zinasema nyumba kadhaa ziliharibika katika mashambulizi hayo.
Mashambulizi hayo yanatokea siku chache baada ya waasi wa Kihouthi wanoungwa mkono na Iran kukiri walishambulia, kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani, bomba la mafuta la Saudi Arabia.
Mashambulizi ya leo yametokea siku moja baada ya mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa (UN) kwa Yemen, Martin Griffiths, kutangaza jana kwamba waasi wa Kihouthi wamehamisha majeshi yao kutoka kwenye mji muhimu wa bandari ya Hodeida.
UN ilikuwa imesema kuwa hiyo ni hatua nzuri kuelekea kupunguza mivutano Katika nchi hiyo ambayo imegubikwa na miaka minne ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.