Watoto waliokuwa wakitafuta kuni nje ya kijiji cha Kabanga jirani na mji wa Mpigi, takribani kilometa 40 magharibi mwa mji mkuu Kampala, walifanya ugunduzi huo wa kutisha siku ya Jumatatu, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.
Polisi wamesema wakazi waliwaambia maafisa kuwa kulikuwa na maboksi yaliyokuwa na vitu vinavyoonekana kuwa mafuvu yaliyozikwa ndani ya jengo la ibada.
“Haraka tuliingia na kuchimba eneo hilo, na mpaka sasa tumepata mafuvu ya binadamu 17” msemaji wa polisi wa eneo hilo Majid Karim alisema.
“Tunafanya uchimbaji zaidi kuhakikisha hakuna mafuvu zaidi kuliko haya tuliyoyagundua” alisema.
Aliongeza kuwa mabaki hayo yanafanyiwa uchunguzi kujua umri wao na jinsia, pamoja na kujua lini yalifukiwa.
Amewasihi watu kuwa watulivu, akisema baadhi ya wakazi wameondoka kwa woga.