Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:16

Mauaji ya msitu wa Shakahola: Familia zaendelea kuomboleza


Wafanyikazi walibeba kwenye mifuko miili ya watu iliyofukuliwa na kuipeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, terehe 25 Aprili 2023. Picha na Yasuyoshi CHIBA / AFP.
Wafanyikazi walibeba kwenye mifuko miili ya watu iliyofukuliwa na kuipeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, terehe 25 Aprili 2023. Picha na Yasuyoshi CHIBA / AFP.

Familia za waathiriwa wa mkasa mbaya kabisa kutokea katika pwani ya Kenya, kwenye shamba la Shakahola ambako watu walidanganywa na mchungaji wao kubaki na njaa hadi kufariki ili kuweza kwenda kukutana na Yesu, wanedelea kuomboleza vifo vya wapenzi wao.

Nyumbani kwa James Tole Mwambela, familia inamuombea ndugu yao Nelson Kimbichi Mwambela. Wanasema hicho ndiyo kitu pekee wanachoweza kukifanya. Ikiwa nii miezi mingi imepita tangu wamuone ndugu yao.

Yote hayo yalianza wakati familia ilipogundua kuwa ndugu yao alikuwa ameacha kuwapeleka watoto wake shuleni, tabia ambayo siyo ya kawaida kwake, kitu ambacho kiliwafanya wajiulize kuhusu hali yake, kaka yake James Mwambela alisema.

"Wakati huo, watu hawakuwa wanajua kuhusu mafundisho ya Mchungaji Paul Mackenzie, wengi wangedhania hivyo, lakini ndugu yangu aliendelea kusema kwamba ulimwengu unaisha, na Yesu anarudi," Yakobo alisema. "Sisi wote hatukukubaliana naye, akiwemo mama na baba yangu."

Mackenzie, kiongozi wa dhehebu la kidini la Good News International Church, alikuwa akionya kuhusu siku ya mwisho, akiyaita maisha katika nchi za Magharibi kuwa ni ya “uovu,” na kusema tiba, elimu, chakula, michezo na burudani kuwa “hazina maana.”

Nelson kisha akaacha kazi aliyokuwa akifanya na kumhamisha mke wake na watoto sita kwa siri kwenda kwenye shamba la Shakahola linalomilikiwa na Mackenzie. Mahali aliko palikuwa siri. Mama yake Nelson, Janet Mwambela, aligundua mapema kuwa kuna kitu si cha kawaida kinachoendelea.

"Inaonekana kama alianza taratibu kuwafundisha watoto jinsi ya kufunga. Kuna wakati, nilimuuliza mwanangu kama alikuwa anakula — alikuwa amekonda sana,” mama yake Nelson aliiambia VOA.

Wanafamilia wakiwa katika msitu wa Shakahola wakisubiri taarifa kuhusu wapendwa wao
Wanafamilia wakiwa katika msitu wa Shakahola wakisubiri taarifa kuhusu wapendwa wao

Maafisa wanasema Mackenzie aliwaambia wafuasi wake wafe njaa ili wakutane na Yesu. Wachunguzi bado wanajaribu kubaini ni watu wangapi walipoteza maisha ambao walikuwa wafuasi wa madhehebu yanayofanana na dhehebu hilo, wakati wakiendelea kufukua makaburi yenye kina kirefu yalioko katika shamba hilo. Idadi ya waliofariki imeongezeka na kufikia zaidi ya 300.

Pia walipata mali binafsi, ikiwemo Biblia ya “Bw. na Bi Nelson Kimbichi Mwambela.” Ni uthibitisho pekee uliopo familia iliyonayo unaothibitisha kuwa Nelson na familia yake walikuwa Shakahola. Hakuna mabaki ya miilli yao imetambuliwa hadi sasa.

Mackenzie kwa sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi akikabiliwa na mashtaka ya kuhubiri imani hatari zilizosababisha vifo vya mamia ya wafuasi wake kufa njaa. Mmoja wa wasaidizi wake , Joseph Juma Buyuka, alifariki wiki hii akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kugoma kula.

Forum

XS
SM
MD
LG