Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:08

Kenya: Mvutano mkali unatarajiwa bungeni wakati mswaada wa fedha wa 2023 ukisomwa


Kikao cha Bunge nchini Kenya
Kikao cha Bunge nchini Kenya

Mvutano mkali unatarajiwa kuwepo katika bunge la kitaifa nchini Kenya wakati Mswaada wa fedha wa mwaka 2023 ukiingia katika hatua yake muhimu ya kusomwa kwa watu Jumanne, Juni 20.

Wabunge wanaoungwa mkono na Kiongozi wa upinzani Raila Odinga wamepanga marekebisho manane kwenye sheria iliyopendekezwa.

Kwa upande wa wabunge wanaoungwa mkono na serikali wakiwa na marekebisho mawili wanayotaka yafanywe kuhusu mswaada huo.

Kiongozi wa wabunge walio wachache bungeni Opiyo Wudanyi amesema bunge linataka kupigia kura mswaada huo kifungu baada ya kifungu ili kurekebisha mapendekezo yenye utata kama vile ushuru wa nyumba kabla ya kupigiwa kura.

Mjadala huo unatarajiwa kuendelea mpaka majira ya usiku wa leo hadi asubuhi kama wabunge watashindwa kukubaliana.

Forum

XS
SM
MD
LG