Ukopeshaji utafanywa kupitia chombo cha mkopo kiitwacho Development Policy Operations (DPO), ambacho kitaifanya Kenya kuanzisha mageuzi yenye lengo la kufungua uwanja wa kifedha, kuboresha ushindani wa kilimo na kuboresha utawala.
"Mageuzi ya serikali, yanayoungwa mkono na DPO, yatasaidia kufanikisha uimarishaji wa sera za serikali zenye lengo la kupunguza nakisi na ulimbikizaji wa deni, kitu ambacho ni muhimu katika kupunguza mzigo wa deni na athari zinazohusiana nazo, kwa usawa na njia endelevu," alisema Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia nchini Kenya, Aghassi Mkrtchyan katika taarifa.
Rais William Ruto, ambaye alichaguliwa mwaka jana, aliahidi kurejesha nidhamu ya fedha katika serikali baada kuongezeka kwa deni la taifa wakati wa utawala wa raisi aliyemtangulia.
Lakini pendekezo lake la kuongeza kodi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiwa ni sehemu ya mswaada wa sheria ya fedha ambao serikali yake itawasilisha bungeni mwezi ujao, mswaada huo umekabiliwa na upinzani kutoka kwa watumishi wa umma na wapinzani wa kisiasa.
Kenya ilipitishwa kupata ufadhili kupitia chombo cha DPO mwaka 2019 na tangu wakati huo nchi hiyo imekuwa ikipokea mikopo kama hiyo minne, mkopo wa mwisho ulikuwa mwishoni mwa Machi.
Uchumi wa Kenya unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.8 mwaka 2023 kutoka asilimia 4.8 mwaka 2022. Benki kuu ya nchi ilisema mwezi Machi.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.
Forum