Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:27

Rushwa yaathiri ukusanyaji kodi Kenya-Ruto


Mfanyakazi akijaza mafuta kwenye gari katika kituo cha mafuta kilichopo Nairobi, mwezi Mei 17 2023. Picha na SIMON MAINA / AFP.
Mfanyakazi akijaza mafuta kwenye gari katika kituo cha mafuta kilichopo Nairobi, mwezi Mei 17 2023. Picha na SIMON MAINA / AFP.

Rais wa Kenya William Ruto siku ya Ijumaa aliwashutumu wafanyakazi wa mamlaka ya kukusanya kodi kwa kukata mapato ya serikali kwa kupokea rushwa na kushirikiana na wakwepa kodi.

Ruto, ambaye alichaguliwa rais mwezi Agosti mwaka jana kwa ahadi ya kuwasaidia maskini, amekuwa akipitia changamoto nyingi katika miezi ya mwanzo ya utawala wake kutokana na kuongezeka kwa ulipaji wa madeni ya serikali, upungufu wa ukusanyaji wa mapato na kuendelea kupanda kwa bei za bidhaa za msingi.

Watumishi wa umma wamekuwa wakilalamikia kuchelewa kulipwa mishahara yao katika miezi ya hivi karibuni wakati mamlaka za serikali za mitaa zimetishia kufunga shughuli zao na kupinga uchelewesho wa kupatiwa pesa za malipo kutoka katika serikali ya kitaifa.

"Udanganyifu, kupokea rushwa na ufisadi wa jumla umetawala shughuli za Mamlaka ya Mapato Kenya (KRA) Ruto aliwaambia wasimamizi wa KRA na wajumbe wa bodi katika hafla iliyorushwa moja kwa moja kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Juhudi za serikali za kuongeza ukusanyaji mapato umetatizwa na wafanyakazi wasio waaminifu wa mamalaka hiyo ya KRA, alisema, ambao hutumia muda wao kuwasaidia mafisadi wanaokwepa kulipa.

KRA ilikataa kutoa maoni.

Mamlaka nchini Kenya zimekuwa zikipambana na ufisadi wakati shirika la kukusanya kodi limekuwa likichunguzwa. Mwezi Mei mwaka 2019, wafanyakazi 75 wa KRA walikamatwa kwa tuhuma za hongo na kuwasaidia wakwepa kodi.

Chanzo cha habari ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG