Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 20:29

Kenya yakanusha ripoti za 'Reuters' kuhusu udukuzi wa China


Treni ikiwa kwa reli ya kisasa ya SGR nchini Kenya.
Treni ikiwa kwa reli ya kisasa ya SGR nchini Kenya.

Afisa mmoja mwandamizi katika wizara ya usalama ya Kenya , Alhamisi alipuuzilia mbali ripoti ya shirika la habari la Reuters, na kuiita ya "propaganda."

Ripoti hiyo ilidai kwamba kulifanyika mfululizo wa udukuzi wa miaka mingi wa majasusi wa mtandao wa China dhidi ya serikali ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Jumatano, shirika la habari la Reuters liliripoti kwamba wadukuzi wa China walifanya msururu wa uvamizi wa kidijitali dhidi ya wizara muhimu za Kenya na taasisi za serikali, kulingana na vyanzo vitatu, ripoti za utafiti wa usalama wa mtandao na uchambuzi wa Reuters wenyewe, wa data zinazohusiana na udukuzi huo.

Vyanzo viwili kati ya hivyo vilitathmini udukuzi huo kulenga habari kuhusu deni ambalo Kenya inadaiwa na Beijing.

"Ripoti hiyo inafaa kuchukuliwa kama propaganda zilizofadhiliwa," Katibu Mkuu wa Usalama wa Ndani na Utawala wa Kitaifa Raymond Omollo alisema katika taarifa ya maandishi, ambayo haikutoa ushahidi wa kuunga mkono madai yake.

Omolo alisema uenezi mpana na shauku ya vyombo vya habari vya kigeni vilivyo na mielekeo inayojulikana zaidi, vinadokeza shambulio lililopangwa na la pamoja dhidi ya uhuru wa Kenya," aliongeza.

Reuters ilisema kampeni ya udukuzi huo imefanyika kwa miaka mitatu , ikilenga wizara nane na idara za serikali ikiwemo ofisi ya rais, hiyo ni kwa mujibu wa mchambuzi wa maswala ya kiinteligensia katika eneo.

Wizara ya mambo ya nje ya china ilisema ilikuwa haifahamu kuhusu udukuzi wowote.

Lakini msemaji wa shirika la habari la Reuters alisema wana imani na uhalisia wa ripoti yao.

Forum

XS
SM
MD
LG