Taarifa hii ni kwa mujibu wa vyanzo vitatu vya habari, utafiti wa usalama wa mtandaoni, na uchambuzi wa reuters wenyewe wa data za kiufundi zinazohusiana na udukuzi huo.
Vyanzo viwili kati ya vinavyotathmini udukuzi huo unalenga angalau kwa kiasi fulani kupata taarifa juu ya deni linalodaiwa na Beijing na taifa hilo la Afrika mashariki.
Kenya ni kiungo cha mkakati katika mpango mradi wa Belt and Road Initiative – wa rais Xi Jinping wa mtandao wa mioundombinu ya kimataifa.
Muafaka zaidi huenda ukapatikana kama moja ya maelewano kwa mikakati ya malipo inayohitajika, ripoti ya julai 2021 iliyoandikwa na mkandarasi wa utetezi kwa wateja wa kibinafsi ilieleza.
Wizara ya mambo ya nje ya china imesema ilikuwa haifahamu kuhusu udukuzi wowote.
Wakati ubalozi wa china nchini uingereza uliziita shutuka hizo haina msingi, ikiongeza kuwa Beijing inapinga na kupambana na udukuzi wa mtandaoni na wizi kwa njia zao zote.
Kampeni ya udukuzi huo imefanyika kwa miaka mitatu , ikilenga wizara nane na idara za serikali ikiwemo ofisi ya rais, hiyo ni kwa mujibu wa mchambuzi wa maswala ya kiinteligensia katika eneo.
Forum