Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 02:06

IMF kuipatia Kenya mkopo mpya wa $1b


PICHA YA MAKTABA: Nembo ya IMF katika makao yake makuu mjini Washington DC, Marekani
PICHA YA MAKTABA: Nembo ya IMF katika makao yake makuu mjini Washington DC, Marekani

Wafanyakazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF,  na Kenya wamefikia makubaliano ambayo yanaweza kufungua zaidi ya dola bilioni 1 ya ufadhili mpya, na ambayo huenda yakapunguza shinikizo la kifedha  katika nchi hiyo yenye  uchumi mkubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kenya imekuwa ikikabiliwa na matatizo ya kifedha kutokana na kuongezeka kwa viwango vya riba ya mikopo ya kimataifa na athari za ukame mbaya zaidi katika miongo minne, ingawa mkurugenzi mkuu wa IMF alisema mapema mwezi huu kwamba hatarajii nchi kushindwa kulipa madeni yake.

IMF ilisema katika taarifa yake Jumanne kwamba mikataba hiyo ilijumuisha ukaguzi wa hivi punde zaidi wa Mpango wa ukopeshaji wa ziada, na Mipango ya Usaidizi wa Kulipa Mikopo, iliyoidhinishwa mwezi Aprili mwaka 2021 katika mpango mpya chini ya Mfumo wa Ustahimilivu na Uendelevu.

IMF Ilikubaliana na maafisa wa Kenya kuongeza muda wa Mpango wa Upanuzi na Usaidizi wa Kuongeza Mikopo kwa muda wa miezi 10, hadi mwezi Aprili mwaka 2025 ili kutoa muda zaidi wa kutimiza masharti yote, na kuongeza kiasi cha pesa kinachopatikana kwa Kenya chini ya mkopo hupo, kwa takriban dola milioni 544.

Kenya pia itapata takriban dola milioni 544 chini ya Mpango wa Ustahimilivu na Uendelevu, ulioanzishwa katika juhudi za kuimarisha ustahimilivu na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

IMF ilisema ufadhili wa jumla uliotolewa kwa Kenya chini ya mpango huo wa mkopo ulifikia takriban dola bilioni 3.5 za Marekani, na kwamba makubaliano ya kiwango cha wafanyikazi yanatarajiwa kujadiliwa na bodi yake kuu, mwezi Julai mwaka huu.

Forum

XS
SM
MD
LG