Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:55

Je, matumaini ya Zimbabwe yakuzindua sarafu mpya ya dhahabu ya kidigitali yatapunguza mahitaji ya dola?


Mfumuko wa bei katika uchumi wa Zimbabwe. Sarafu ya dhahabu ya kidigitali kuchukua nafasi ya dola kuimarisha uchumi wa Zimbabwe.
Mfumuko wa bei katika uchumi wa Zimbabwe. Sarafu ya dhahabu ya kidigitali kuchukua nafasi ya dola kuimarisha uchumi wa Zimbabwe.

Benki Kuu ya Zimbabwe Mei 8 ilizindua sarafu mpya ya dhahabu ya kidigitali ikiwa na matumaini  itapunguza mahitaji ya dola ya Marekani na kushuka thamani kwa dola ya Zimbabwe.

Lakini wachambuzi wanasema soko la kubadilisha fedha za kigeni ambalo linadhibitiwa na serikali ndiyo linachochea tatizo.

Zimbabwe ilianza kutumia tena sarafu yake mwaka 2019 lakini hivi sasa thamani iko katika zaidi ya 2,000 kwa dola moja ya Marekani kwenye soko la magendo.

Serikali ina matumaini ya kuiachia sarafu ya dhahabu ya digitali ambayo itapunguza kushuka haraka thamani kwa dola ya Zimbabwe.

Mthuli Ncube, Waziri wa Fedha wa Zimbabwe anasema “ni jambo zuri sana. Hizi sarafu za digitali zinasaidia na hasa dhahabu yenyewe katika biashara ya kila siku, kwahiyo ni kitu cha uhakika. Kwahiyo mtu yeyote anayetaka kufanya ununuzi atajihisi yuko vizuri kufanya hivyo kwa kutumia dhahabu ambayo itahifadhi thamani.”

Makampuni ya kununua sarafu mpya ya digitali yana matumaini itaweza kulinda uwekezaji wao kwa sarafu ya ndani.

“Tuna kiwango kikubwa kiasi cha uwekezaji kwa fedha za ndani, hasa katika soko la fedha. Baada ya kutathmini pendekezo kutoka Benki Kuu, haraka tuligundua kwamba ni njia muafaka sana. Kwasababu inahusishwa na mali ambazo ni dhahabu na itakulinda katika misingi ya kushuka kokote kwa thamani ya sarafu,” anasema Farai Gwaka wa Zimnat Asset Management.

Lakini katika maoni ya maandishi kwa VOA, ofisi ya Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) nchini Zimbabwe lilielezea wasi wasi wake kuhusu sarafu ya digitali na udhibiti wa soko.

IMF imesema tathmini ya uangalifu mkubwa inahitajika ili kuhakikisha faida ya sarafu mpya inazidi gharama na hatari zinazoweza kujitokeza.

Wachumi wanasema kuwa na dhahabu ya kutosha kutasaidia kuondoa wasi wasi unajitokeza.

Mchumi wa maendeleo, Prosper Chitambara anasema, “kimakaratasi. Nasema sarafu ya dhahabu ya digitali kwa kweli ni wazo zuri kiuchumi. Lakini nadhani uwazi zaidi unahitajika katika misingi ya masuala ya hifadhi, ni akiba ya dhahabu ya kiasi gani cha dhahabu katika nchi, ili kufanikisha kutetea sarafu hizi za dhahabu.”

Vyombo vya habari vya Zimbabwe mwezi Aprili viliripoti kuwa serikali ilikuwa na kiasi cha dhahabu yenye thamani ya dola milioni 23 na ilipanga kuweka akiba ifikie mpaka dola milioni 100.

Mwaka jana Zimbabwe iliitangaza sarafu ya dhahabu kujaribu kuleta uthabiti katika dola yake, lakini sarafu tangu wakati huo imeshuka thamani kwa chini ya theluthi.

Wachambuzi wanasema tatizo kubwa ni udhibiti wa Zimbabwe kwenye soko la sarafu, ambalo linathamini dola ya Zimbabwe kwa zaidi ya mara sita ya kiwango cha biashara kwenye soko la magendo.

XS
SM
MD
LG