Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:32

Wauguzi nchini Zimbabwe sasa kuhukumiwa jela ikiwa watagoma


Serikali ya Zimbabwe imepitisha mswaada wa sheria Jumanne Januari 10 inayopiga marufuku maandamano  yaliyoandaliwa na wafanyakazi wa afya nchini humo kufuatia mgomo katika mzozo wa muda mrefu kuhusu malipo.

Kwa mujibu wa Sheria hiyo mpya iliyosainiwa na Rais Zimbabwe Emmerson Mnangagwa mapema wiki hii, sheria hiyo inapiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na wahudumu wa afya nchini Zimbabwe na kuchukuliwa ni kosa la jinai hiyvo kuwafanya waandamanaji kukabiliwa na adhabu ya faini au kifungo cha mpaka miezi sita jela.

Sheria hiyo mpya inakuja baada ya vuta nikuvule ya mzozo wa muda mrefu baina na wahudumu wa afya na serikali kuhusu mishahara.

Maelfu ya wauguzi na madaktari katika hospitali zinazosimamiwa na serikali waligoma mwaka jana, na katika miaka ya nyuma, wakidai nyongeza ya mishahara na kutaka kulipwa mishahara hiyo kwa dola za Kimarekani.

Hiyo inatokana na kushuka thamani kwa sarafu ya nchi hiyo na kupanda kwa mfumuko wa bei ulioshusha thamani ya mapato yao kama anavyoeleza Pretty Gudza mmoja wa wauguzi walioandamana.

"Siwezi kulipa kodi yangu, siwezi kula, kwa hivyo hali zetu ni mbaya na sababu ya kufanya mgomo huu ina uhalali," anasema muuguzi Gudza.

Wauguzi wengi nchini Zimbabwe wanalipwa chini ya dola 100 kwa mwezi.

Taifa hilo la Kusini mwa Afrika limeshuhudia idadi kubwa ya wauguzi na madaktari wanaoondoka hatua ambayo imesababisha hospitali kukosa wafanyakazi.

Mnamo Novemba mwaka 2022 Bodi ya Huduma za Afya ya Zimbabwe ilisema zaidi ya wafanyakazi 4,000 wa afya wameondoka nchini humo tangu 2021.

XS
SM
MD
LG