Kwa sasa, Wizara ya Elimu ya Msingi na Sekondari nchini humo imeimarisha kinga dhidi ya ugonjwa huo ili kuepusha mlipuko mkubwa zaidi mashuleni.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto lildai kuwa umaskini, majanga ya kiasili, migogoro, mabadiliko ya hali ya hewa na ukosefu wa maji salama na usafi wa mazingira vimechangia zaidi janga la kipindupindu barani Afrika.