Zimbabwe inaelekea kwenye uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu ukitarajiwa kuwa wenye ushindani mkubwa, wakati chama ZANU-PF tayari kikilaumiwa kuzima sauti za upinzani. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, baadhi ya wapiga kura katika siku 5 zilizopita wamedai kupojea ujumbe unaoisifu serikali kwenye simu zao za mkononi.
Ujumbe wanaopokea unasemekana kuandikwa kwa lugha ya kishona, ukijumuisha jina la mwenye simu, wilaya yake na kutiwa saini ya “ Rais ED Mnangagwa”. Kundi la wanaharakati la Team Pachedu, linailaumu tume ya uchaguzi ya Zimbabwe ZEC, kwa kutoa taarifa za wapiga kura kwa chama tawala cha ZANU-PF, ukiwa ukiukwaji mkubwa wa usiri wa watu pamoja na sheria za uchaguzi.