Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:39

Kenya yasaini Mkataba wa kiuchumi na Umoja wa Ulaya



Mkulima wa kahawa Josphat Muchiri akiwa katika shamba la kahawa huko Kiambu Kenya, tarehe 2 Agosti, 2019. Picha na TONY KARUMBA / AFP.
Mkulima wa kahawa Josphat Muchiri akiwa katika shamba la kahawa huko Kiambu Kenya, tarehe 2 Agosti, 2019. Picha na TONY KARUMBA / AFP.

Kenya na Umoja wa Ulaya zimetia saini Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) ambao nchi hiyo inalenga kuutumia kupanua mazuo yake ya nje kwenye soko la Ulaya.

Mkataba huo ambao ulitiwa saini siku ya Jumatatu, unaweka kasi ya ufanyikaji wa biashara, na pia fursa za ufikiaji wa bidhaa za Kenya kwenye nchi za Umoja wa Ulaya bila ya kutozwa ushuru wa forosha wala kuwekewa ukomo wa kiasi cha kuuza. Mkataba huo umechukua takriban miaka saba kukamilishwa.

Mkataba utaanza kutumika baada ya kufanyiwa marekebisho ya kisheria na kisha kutafsiriwa kabla ya Tume ya Umoja wa Ulaya kuwasilisha katika Baraza la Ulaya ili kutiwa saini.

Baadaye Umoja wa Ulaya na Kenya zitatakiwa kutia saini makubaliano hayo ili kuidhinishwa na Bunge la Ulaya. Kuweka nafasi ya kutumika kikamilifu na kutekelezwa na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Umoja wa nchi za Ulaya na Kenya zitahitahitajika kutia saini makubaliano hayo ili kuidhinishwa na Bunge la Ulaya. Kuweka nafasi ya kutumika kikamilifu na kutekelezwa na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Hata hivyo, Rais wa Kenya William Ruto ameeleza kuwa Kenya imejiweka katika nafasi bora kuongeza biashara zake katika soko la Umoja wa Ulaya katika kuzalishaji wa nafasi mpya za ajira, kupanua mapato ya taifa na kuchochea ukuaji endelevu wa uchumi wa nchi.

Umoja wa Ulaya ni kituo cha kwanza cha mauzo ya nje cha Kenya na mshirika wa pili wa kibiashara kwa ukubwa baada ya Benki ya Dunia. Rais Ruto amefafanua kuwa Mkataba huu umebuniwa ili kuchochea biashara na uwekezaji, utengenezaji na huduma zinazoongozwa na mauzo ya nje.

Valdis Dombrovskis, Makamu wa Rais wa Tume ya Ulaya na Kamishna wa Biashara wa Umoja huo ameeleza kuwa Umoja wa Ulaya unalenga kuondoa vikwazo vya kiuchumi na kisiasa kuwekeza zaidi barani Afrika na mkataba huu na Kenya ni kichocheo kikubwa cha kuongezeka kwa biashara.

Mauzo ya kiasi kikubwa ya Kenya kwenye soko la Umoja wa Ulaya ni bidhaa za kilimo kama vile mboga, matunda, chai na kahawa. Zaidi ya asilimia 70 ya maua yaliyokatwa nchini Kenya yanapelekwa kwenye soko la Ulaya.

Mfanyabiashara wa maua, akiuza maua ya Waridi Siku ya Wapendanao huko Nairobi. Picha na SIMON MAINA / AFP.
Mfanyabiashara wa maua, akiuza maua ya Waridi Siku ya Wapendanao huko Nairobi. Picha na SIMON MAINA / AFP.

Kupitia mkataba huo, wakulima wa Kenya wataongeza kipato na kupata uendelevu wa soko linalotabirika hasa kwa samaki, mboga, matunda, maua, chai na kahawa.

Aidha, mkataba huo unazihimiza sekta binafsi za Umoja wa Ulaya kuwekeza nchini Kenya na kuchochea uzalishaji wa ajira katika sekta mbalimbali.

Sam Okumu, mtaalam wa biashara, uchumi na uwekezaji nchini Kenya, anaeleza kuwa hii ni hatua bora kwa Kenya kuingia katika soko la Umoja wa Ulaya.

Mkataba huu ni kilele cha mazungumzo ya kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyoanza miaka saba iliyopita. Mwaka 2014, licha ya Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi na Rwanda kukamilisha mazungumzo ya makubaliano haya ya kiuchumi, ni Kenya pekee iliyosonga mbele kwa kasi na kuuidhinisha mkataba huo kikamilifu.

Rais wa Kenya William Ruto aliongoza hafla iliyofanyika jijini Nairobi ikiashiria kukamilika rasmi kwa mashauriano ya Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya EU na Kenya.

KENNEDY WANDERA, SAUTI YA AMERIKA, NAIROBI.

Forum

XS
SM
MD
LG