Kenya : Watu wasiopungua 15 wafariki, sababu ya ajali yaelezwa

Ramani ya Kenya

Polisi katika kaunti ya Kilifi Pwani ya Kenya wanasema watu wasiopungua 15 wamefariki kutokana na ajali ya mabasi mawili ya abiria mapema Jumatano kwenye barabara kuu kati ya mji wa kitalii wa Malindi, na Mombasa.

Mkuu wa utawala wa kaunti ya Kilifi Kutswa Olaka anasema ajali ilitokea baada ya tairi la basi moja kupasuka na kugongana na basi dogo likitokea Malindi kuelekea Mombasa.

Mkuu wa utawala wa kaunti ya Kilifi Kutswa Olaka anasema ajali imetokea katika njia panda kati ya Malindi na Garisa na kwamba zaidi ya watu 20 wamejeruhiwa baadhi wakiwa katika hali mahtutii na kupelekwa kwenye hospitali mbalimbali za kaunti hiyo.

Waliofariki ni pamoja na madereva wa mabasi hayo mawili, moja likitoka Mombasa kuelekea Garisa na basi dogo likitokea mainland kuelekea Mombasa.

Mkuu wa polisi wa Kilifi kamanda Nelson Tait amewaonya madereva kuchukua tahadhri zaidi barabarani.

Kwa pande wao wakazi wa Eneo hlo anaomba wakuu wa serikal kupanua barabara katika aneo hlo ambako kumeokea ajali nyng kama anavyoeleza Joseph maina kwa waandshi habari.