Kenya: IEBC yasema wapiga kura laki 250 waliokufa wameandikishwa

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati, Nariobi, Kenya.

Tume ya uchaguzi nchini Kenya inasema ukaguzi unaoendelea  katika daftari la wapiga kura umegundua kuwa kuna karibu wapiga kura 250,000 waliokufa ambao wameandikishwa.

Karibu nusu milioni ya wapiga kura wamegundulika kuwa wameandikishwa zaidi ya mara moja na watu 226,000 wameandikishwa kwa kutumia nyaraka ambazo siyo za kwao.

Wengine wanajiandikisha kwa kutumia nyaraka zisizo sahihi , tume ya IEBC imesema katika taarifa yake ambayo inaonyesha kuwa watu zaidi ya milioni moja wameathiriwa. Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amesema kwa sababu ya utekelezaji wa matokeo ya ukaguzi wa awali tume itachelewesha uidhinishaji wa mwisho kwa ajili ya kuchapisha.

Hapo awali tume hiyo ilisema kwamba itachapisha orodha ya wapiga kura kabla ya june tisa lakini imesogeza mbele tarehe hiyo hadi juni 20 wakati inashughulikia matokeo ya KPMG shirika lililopewa kazi ya kufanya ukaguzi huo.

Wagombea wanne katika uchaguzi wa Augusti 9 wamepitishwa kuwania nafasi ya urais akiwemo David Mwaure, George Wajackoyah, Raila Odinga na William Ruto.