Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:21

Rais Kenyatta avunja kanuni na kumnyima naibu wake fursa ya kuhutubia taifa


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, akiwa na naibu wake Dr. William Ruto. July 21, 2015. PICHA: AP
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, akiwa na naibu wake Dr. William Ruto. July 21, 2015. PICHA: AP

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekataa kumpa fursa naibu wake kuhutubia taifa katika maadhimisho ya siku ya Madaraka.

Hii ni mara ya Kwanza Ruto amekosa kupewa fursa ya kuhutibia taifa tangu Kenyatta alipoingia madarakani mwaka 2013.

Hatua ya Kenyatta imetafsiriwa na raia wa Kenya kama kilele cha tofauti kati ya Ruto na Kenyatta, ambao hivi karibuni walikosa kukaa kwenye meza moja wakati wa maombi ya kitaifa.

Wakenya ambao walitarajia kumsikiliza naibu wa rais William Ruto, wakati wa maadhimisho ya mwisho ya siku ya Madaraka, badala yake wameshuhudia rais Kenyatta akivunja kanuni na kuanza kuhutubia taida baada ya kutoa tuzo za kitaifa na kumwalika rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio.

Kabla ya hapo, rais Kenyatta aliongoza kikao cha baraza la mawaziri akiwa na mke wake Margaret Kenyatta, bila ya kumwalika Ruto.

Katika kikao cha baraza la mawaziri, Kenyatta ameshukuru mawaziri wake kwa kushirikiana naye, na kusema kwamba alikuwa na Imani kwamba ameweka msingi imara kwa viongozi watakaoingia madarakani baada yake.

Kiongozi wa chama cha Orange democratic movement, na ambaye ni mgombea wa rais anayeungwa mkono na rais Kenyatta, Raila Odinga, pamoja na mgombea wake mwenza, wamehudhuria sherehe za Madaraka.

Sherehe ya leo imekuwa ya mwisho ya kitaifa kwa rais Kenyatta, kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti tarehe 9.

Wafuasi wa William Ruto, anayegombea urais, wametaja hatua ya rais Uhuru Kenyatta kumuunga mkono Raila Odinga katika uchaguzi wa urais, kuwa usaliti.

XS
SM
MD
LG