Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:13

TikTok yashtumiwa kusambaza matamshi ya chuki na habari potofu kabla ya uchaguzi wa Kenya


Nembo ya App ya TikTok, picha ya AP
Nembo ya App ya TikTok, picha ya AP

Kanda zenye matamshi ya chuki, habari potofu za kisiasa na vitisho vya ghasia za kikabila zinasambaa kwenye mtandao wa TikTok kabla ya uchaguzi muhimu nchini Kenya, ripoti mpya imesema Jumatano, ikilishtumu jukwaa hilo kushindwa kuzuia usambazaji wa kanda hizo za video.

Taifa hilo lenye uchumi mkubwa Afrika mashariki litaanda uchaguzi wa rais na bunge tarehe 9 Agosti, huku kukiwa na kumbukumbu mbaya za uchaguzi wa awali ambao uligubikwa na ghasia za kikabila.

Jumatano, taasisi ya kimataifa Mozilla yenye makao yake Marekani imesema ilichunguza video 130 ambazo zilikuwa na lengo la kueneza habari potofu na kuzua hofu, na zilitizamwa na zaidi ya watu milioni 4 baada ya kusambazwa na darzeni ya akaunti kwenye mitandao ya kijamii.

“Demokrasia ya Kenya ina historia chafu ya ghasia za baada ya uchaguzi. Sasa, taarifa potofu za kisiasa kwenye TikTok, ikikiuka sera zake ilizoweka, zinachochea hali hii ya kisiasa inayotisha,” amesema Odanga Madung kutoka taasisi hiyo.

Video nyingi zilikuwa na vitisho vya ghasia za kikabila dhidi ya jamii zinazopatikana katika eneo la Bonde la Ufa, kwa mujibu wa taasisi hiyo.

Katika mfano mmoja, video moja ambayo ilitizamwa na zaidi ya watu 400,000, ilidai kwamba kuna mgombea urais ambaye anachukia kabila fulani na atawalenga watu wa kabila hilo ikiwa ataingia madarakani.

Msemaji wa TikTok ameiambia AFP kwamba kampuni hiyo inapanga kuweka kanuni mpya ili kuwaunganisha watumiaji wa mtandao huo na habari zenye uhakika kuhusu uchaguzi wa Kenya.

“Tunakataza na kuondoa taarifa potofu za uchaguzi, kuhamasisha vurugu, na ukiukaji mwingine wa sera zetu,” amesema.

XS
SM
MD
LG