Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 05:38

IEBC: Musyoka hatashiriki kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais Kenya, Agosti 9


Kalonzo Musyoka
Kalonzo Musyoka

Kiongozi wa Chama cha Wiper nchini Kenya, Kalonzo Musyoka hatashiriki katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Rais Agosti 9 baada ya tume ya uchaguzi ya nchi hiyo  kumzuia kugombea kutokana na utaratibu uliopo.

Wakati huo huo, Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) imewapitisha wagombea 16 ambao hivi sasa watawasilisha nyaraka zao za uteuzi wao kuanzia Jumamosi.

Orodha hiyo ina wagombea watarajiwa 9 wa vyama vya siasa au muungano wa vyama vya kisiasa na wagombea saba huru.

Wagombea wanaoongoza Raila Odinga wa Azimio la Umoja (One Kenya Coalition party) na Naibu Rais William Ruto wa Chama cha United Democratic Alliance ni kati ya waliopitishwa na IEBC.

Bwana Musyoka hakuwasilisha orodha ya wafuasi wake katika waraka wa Microsoft Excel.

Yeye ni miongoni mwa wagombea wanne wa vyama vya siasa na tisa wagombea huru walioshindwa kukidhi matakwa ya IEBC ya kupata wafuasi 48,000 na angalau kaunti 24, kuwasilisha majina ya wafuasi hao pamoja na nakala ya vitambulisho vyao vya kitaifa.

Kwa Bw Musyoka, kushindwa kwake kuvuka kiunzi cha kwanza kunahitimisha safari yake ya ugombea urais ambayo ilianza baada ya kushindwa kupata nafasi ya mgombea mwenza wa Chama cha Azimio.

Hata kabla ya kujulikana kuwa amezuiwa kushiriki katika kinyang’anyiro hicho na IEBC, wafuasi wa Bw Musyoka na wagombea wa Wiper walikuwa wanaweka shinikizo kwake kurejea katika chama cha Azimio na kuwaunga mkono Odinga -Martha Karua.

Hivi sasa yeye hana hiari kwani kisheria hawezi tena kutoka Azimio.

Lakini tayari yuko mashakani wakati akijaribu kujiunga tena na chama cha Azimio la Umoja One Kenya Coalition.

XS
SM
MD
LG