Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:54

Kenya: Ruto amuomba Kenyatta msamaha


Rais Uhuru Kenyatta (Kulia) na Makamu wake William Ruto, Nairobi, Kenya.
Rais Uhuru Kenyatta (Kulia) na Makamu wake William Ruto, Nairobi, Kenya.

Naibu Rais wa Kenya William Ruto amemuomba Rais Uhuru Kenyatta msamaha baada ya viongozi hao kutumbukia katika mvutano baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2018.

Tofauti baina ya Rais Kenyatta na msaidizi wake zimeonekana wazi hadharani.

Rais hamuungi mkono bwana Ruto katika nia yake ya kuwania urais mwezi August mwaka huu, na badala yake ameweka nguvu zaidi kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Bwana Ruto alitoa maelezo yake katika sala ya kila mwaka ya taifa inayojulikana kama Prayer Breakfast iliyoandaliwa na bunge na bwana Kenyatta akiwemo katika ushiriki wa sala hiyo.

Naibu rais alihutubia mkusanyiko wa watu akiomba msamaha kwa wakenya kwa makosa yoyote yaliyofanywa na serikali na baadae alimgusia bwana Kenyatta kama rafiki mzuri.

Rais Kenyatta anayemaliza muhula wake wa pili na wa Mwisho hakujibu lolote kuhusu maelezo ya bwana Ruto.

XS
SM
MD
LG