Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 18:38

Kenya: Odinga amteua Martha Karua Kama mgombea mwenza


 Martha Karua na Raila Odinga.
Martha Karua na Raila Odinga.

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Kenya, ODM, ndani ya muungano wa kisiasa wa Azimio La Umoja Raila Odinga amemteua kiongozi wa Narc-Kenya, Martha Karua awe mgombea mwenza wake kwelekea kwa uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022.

Akizungumza katika Ukumbi wa Kimataifa wa Kenyatta jijini Nairobi (KICC), Raila amemtaja Karua kama mtu mwenye rekodi thabiti ya kutetea haki za binadamu.

"Baada ya tathmini ya kina, tumeamua kwamba tutamteua mwanamke kwa nafasi ya mgombea mwenza," amesema Odinga.

“Nilimtaka mtu mkakamavu na baada ya kupiga darubini na kufanya mashauriano ya kina, nimeamua huyu mtu awe ni mwanamke,” Raila amesema.

Bi Karua, ambaye kwa wakati mmoja aligombea urais wa taifa hilo la Afrika Mashariki, anafahamika na wengi kama mmoja wa wanasiasa wachache wanaochukua misimamo bila kujali athari zake.

Kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika bustani za Kenyatta International Conference Centre, Karua amekubali wajibu aliotwikwa na mgombea wake mkuu na vile vile akapongeza jopo lililosimamia mchakato mzima.

“Ninapongeza jopo la Azimio la Umoja kwa kuendesha shughuli muhimu kwa uwazi hadi mwishowe akapatikana mgombea mwenza. Ninawapongeza wenzangu waliomezea mate nafasi hii,” amesema Karua.

XS
SM
MD
LG