Mji huo wa pwani ulilengwa na wana jihadi wiki mbili zilizopita. Brigadia Chongo Vidigal, msemaji wa jeshi ambaye alizungumza na wanahabari Ijumaa jioni amesema kuwa idadi ya waliouawa huenda ikawa kubwa zaidi.
Vidigal amesema serikali inaamini kwamba jeshi kuingilia kati huko Palma kumekuwa na mafanikio.
Wanamgambo wenye uhusiano na Islamic State wameshambulia mji wa pwani wa kaskazini mashariki wa Palma March 24, na kuharibu majengo na kuwakata vichwa raia.
Wanamgambo hao ambao wanajulikana kama al-Shabaab hawana uhusiano na kundi kama hilo nchini Somalia.
Wanamgambo hao wa Cabo Delgado wamefanya mlolongo wa uvamizI kwenye miji na vijiji ikiwa ni juhudi ya kusimika ukhalifa wa Kiislamu. Bado haiko bayana raia wangapi wameuawa.