Jenerali Mark Milley aonya uharibifu utakaoletwa na maamuzi ya Russia

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na Jenerali Mark Milley wakijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya mgogoro kati ya Russia na Ukraine, Pentagon, Washington, Jan. 28, 2022.

Afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Marekani ameonya Russia itawasha moto wa mauti na uharibifu, kwa pande zote, iwapo itaamua kutatua tofauti zake na Ukraine kwa kutumia nguvu za kijeshi.

Mwenyekiti wa Wakuu wa Wafanyakazi wa Vikosi vya Majeshi Jenerali Mark Milley ameeleza bayana kukerwa siku ya Ijumaa wakati wa mkutano nadra wa waandishi wa habari huko Pentagon akiwa na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin, ambapo wote walisisitiza janga hili linaweza kuepukwa kama Moscow itakuwa tayari kurudi kutoka kwenye eneo hilo.

“Kuwepo aina ya majeshi yaliyojipanga, mbinu za majeshi ya ardhini, makombora, mizinga, majeshi ya anga, yote hayo yamekusanyika pamoja, kama yataelekezwa kwa Ukraine, itakuwa hali ngumu, ngumu sana,” Milley aliwaambia waandishi.

“Itasababisha vifo vya viwango vikubwa. Unaweza kufikiria hicho hali itaonekana vipi katika maeneo ya mijini yenye watu wengi,” alisema. “Itakuwa ni jambo la kutisha. Itakuwa kitu kibaya. Hakuna haja ya hilo kutokea.”

Onyo lililotolewa na Marekani Ijumaa limekuja wakati kuna mivutano kati ya Russia na Ukraine inayoonekana kufikia hatua ya vita.

Baadaye Ijumaa, Rais Joe Biden aliwaambia waandishi ataongeza wanajeshi wa Marekani katika vikosi vya NATO huko Ulaya Mashariki.