Moscow imeweka zaidi ya wanajeshi 100,000 karibu na mpaka na Ukraine na Marekani ilisema siku ya Ijumaa kuwa inahofia Russia ilikuwa inaandaa kisingizio cha kuivamia iwapo diplomasia itashindwa kufikia malengo yake.
Canada, yenye wakazi wengi na wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa wa asili ya Ukraine, imechukua msimamo mkali na Moscow tangu kujiingiza huko Crimea mwaka 2014.
Kupelekwa kwa wanajeshi na vifaa vya Russia ndani na kuzunguka Ukraine kunahatarisha usalama katika eneo lote. Hatua hizi za kichokozi lazima zizuiwe, Joly alisema katika taarifa yake.