Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:37

Marekani iko tayari kukabiliana na hali yoyote ya dharura Ukraine


Jake Sullivan
Jake Sullivan

Mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani Jake Sullivan, amesema Marekani imejitayarisha kuendelea kuchukua hatua za kidiplomasia kwa nia njema na kujibu vitendo vya Russia nchini Ukraine.

Sullivan amesema kwamba kile wanachoweza kufanya ni kujitayarisha, na kwamba wapo tayari. Amekuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya wiki nzima ya mazungumzo kati ya Marekani, washirika wake na Russia.

Rais Biden na Rais Putin wafanya mazungumzo kwa njia ya mtandao.
Rais Biden na Rais Putin wafanya mazungumzo kwa njia ya mtandao.

Sullivan: "Tumejitayarisha kuendelea na hatua za kidiplomasia ili kuimarisha utulivu na usalama Ulaya na sehemu ya Atlantic. Vile vile tumejitayarisha iwapo Russia itaamua kuchukua njia tofauti. Tunaendelea kushirikiana kwa kiwango kikubwa na washirika wetu kuhusu hatua kadhaa za kiuchumi tutakazochukua iwapo Russia inaivamia Ukraine. Tunaendelea kufanya kazi na washirika wetu wa NATO kuhusu uwezo wetu wa kujibu hatua za Russia endapo zitatokea.

Pia Sullivan ameongeza kusema: "Wazungumzaji tofauti wameonya dalili za matumaini wiki hii. Unaweza kuwauliza msimamo wao kuhusu suala hili. Kwa mtazamo wetu tunaweza tu kuwa wazi kuhusu msimamo wetu ambao ni kwamba tupo tayari kuchukua hatua za kidiplomasia na tayari kujibu uchokozi wa aina yoyote.

Sergei Ryabkov
Sergei Ryabkov

Russia imesema haioni msingi wowote wa kuendelea na mazungumzo na Marekani na NATO, wakati muungano huo unatafuta kuzuia uvamizi wa pili wa Moscow dhidi ya Ukraine.

Akizungumza kwenye televisheni ya Russia, naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Ryabkov, amesisitiza kwamba Marekani na washirika wake wamekataa matakwa ya msingi ya Moscow kwa NATO kukataa uanachama wa Ukraine na mataifa mengine ya kisoviet.

XS
SM
MD
LG