Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 07:47

Marekani kujibu Russia vipasavyo endapo itavamia Ukraine


Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza kwa simu na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza kwa simu na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy

Rais wa Marekani Joe Biden amemueleza rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy kwamba Marekani na washirika wake watajibu inavyostahili, endapo Russia itaivamia Ukraine.

Katika mazungumzo ya simu, viongozi hao wawili wamezungumzia juhudi za kidiplomasia katika kumaliza mgogoro unaotokana na Russia kuendelea kuimarisha juhudi zake za kijeshi kwenye sehemu za mashariki mwa mpaka na Ukraine.

Biden na Zelenskiy wamezungumzia hatua zinazostahili kuchukuliwa kumaliza hali ya wasiwasi katika sehemu ya Donbas na kuhakikisha kwamba makubaliano ya Minsk yanatekelezwa.

Hata hivyo, Biden amesisitiza kwamba Marekani inazingatia sana uhuru wa Ukraine.

Zelenskiy ameandika ujumbe wa Twiter kwamba viongozi hao wawili wamezungumzia hatua za Pamoja kati ya Ukraine, Marekani na washirika wao, katika kuhakikisha kwamba kuna amani Ulaya na kuzuia migogoro.

Biden amepiga hatua ndogo sana katika kumtaka rais wa Russia Vladmir Putin kuondoa wanajeshi wake 100,000 ambao wamepiga kambi kwenye mpaka na Ukraine, japo maafisa wa Marekani wanasema kwamba hawaamini kuwa Putin ameamua kuivamia Ukraine.

Mchambuzi wa siasa za Kyiv Petro Burkovskiy, amesema kwamba rais wa Russia Vladimir Putin ameonyesha kwamba yupo tayari kutoheshimu vikwazo vya nchi za magharibi iwapo ataivamia Ukraine.

XS
SM
MD
LG