Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 23:49

Biden na Putin kufanya kuwasiliana kwa simu Alhamisi


Rais wa Russia Vladimir Putin kushoto, na mwenzake wa Marekani Joe Biden
Rais wa Russia Vladimir Putin kushoto, na mwenzake wa Marekani Joe Biden

Ikulu ya Marekani imesema Jumatano kwamba Rais Joe Biden atazungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Russia Vladimir Putin  Alhamisi.

Hayo yanajiri wakati Washington pamoja na washirika wake wakijaribu kutafuta majibu ya pamoja kuhusiana na kuongezwa kwa wanajeshi wa Russia karibu na mpaka wa Ukraine.

Mkuu wa baraza la kitaifa la usalama la Marekani Emily Home kupitia taarifa amesema kwamba viongozi hao watajadili masuala kadhaa muhimu ikiwemo diplomasia. Ameongeza kusema kwamba Biden amekuwa akishauriana na viongozi wa Ulaya wakati maafisa wa utawala wake wakishauriana na NATO, Umoja wa Ulaya pamoja na baraza la usalama na ushirikiano la Ulaya, OSCE.

Moscow imezua hali ya wasi wasi baada ya kupeleka maelfu ya wanajeshi wake kwenye mpaka wa Ukraine katika kipindi cha miezi miwili iliopita. Mwaka wa 2014,Russia ilijichukulia peninsula ya Crimea ya Ukraine pamoja na kuunga mkono waasi wanaopigana na wanajeshi wa Kyiv mashariki mwa Ukraine.

Msemaji wa Kremlim Dmitry Peskov amesema mawasiliano kwa njia ya video kati ya Putin na Biden yamepangwa kufanyika mida ya jioni.

XS
SM
MD
LG