Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 05, 2025 Local time: 01:11

NATO yajizatiti kwa kupeleka wanajeshi na vifa vya kivita Ukraine


Rais wa Russian Vladimir Putin
Rais wa Russian Vladimir Putin

Jumuiya ya Kujihami ya nchi za Magharibi, NATO, imesema Jumatatu inaweka wanajeshi tayari na kuimarisha upande wa mashariki mwa Ulaya kwa meli zaidi na ndege za kivita ili kujibu hatua ya Russia kuongeza idadi ya wanajeshi katika mpaka wa Ukraine.

Hatua hiyo imeongeza ishara kwamba nchi za magharibi zinajitayarisha kwa uchokozi wa Russia dhidi ya Ukraine, ingawa Moscow inakanusha mpango wowote wa kuvamia.

Uingereza ilisema inaondoa baadhi ya wafanyakazi wake na familia zao katika ubalozi wake huko ukraine ili kujibu tishio kubwa linaloongezeka kutoka Russia, siku moja baada ya Marekani kusema kuwa inaziamuru familia za wanadiplomasia kuondoka.

Ubalozi wa Marekani umesema katika taarifa yake kwamba hatua za kijeshi za Russia zinaweza kuja muda wowote.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba maafisa hawataweza kuwaondoa Wamarekani, kwa hiyo wale walioko Ukraine wajipange ipasavyo.

Hata hivyo wanadiplomasia Wamarekani huko Kyiv wameruhusiwa kuondoka kwa hiari yao .

XS
SM
MD
LG