Russia Jumatano ilikataa matarajio ya vikwazo vya Marekani dhidi ya Rais Vladmir Putin mojawapo ya majibu kadhaa yaliyopendekezwa kama majeshi ya Russia yangeivamia nchi jirani ya Ukraine.
Msemaji wa Kremlin, Dmitri Peskov aliwaambia waandishi wa habari kwamba vikwazo hivyo havitaleta maumivu ya kisiasa lakini vitaleta uharibifu.
Rais wa Marekani Joe Biden siku ya Jumanne alionya kuhusu madhara makali na makubwa kwa Putin, ikiwa ni pamoja na vikwazo binafsi dhidi ya Putin mwenyewe, kama kiongozi huyo wa Russia anawaweka wanajeshi 127,000 ambao wako tayari kushambulia mpaka wa Ukraine.