Je mtu yeyote anaweza kuwa rais wa Marekani?⁣

Your browser doesn’t support HTML5

Hapana.⁣ Kazi iko wazi kwa wale wana sifa zilizotajwa katika Katiba ya Marekani.⁣

Mahitaji:⁣
Awe na Umri wa miaka 35⁣
Awe ameishi ndani ya Marekani kwa miaka 14.⁣
Awe raia mzaliwa wa Marekani.⁣
Wasisi wa taifa walikuwa na matumaini umri huenda ukaleta busara na ukomavu.⁣
Wakati Katiba ilipokuwa inapitishwa umri wa kuishi ulikuwa chini ya miaka 40⁣
Ukazi na uraia:⁣
Mahitaji haya yalikuwa na azma ya kukatisha ushawishi wa nje.⁣
Wataalamu wa kisheria wanaamini uraia wa kuzaliwa unahusu mtu aliyezaliwa nchini Marekani au aliyezaliwa na wazazi ambao ni Wamarekani.⁣
Lakini Mahakama ya Juu Marekani haijawahi kutoa maamuzi rasmi kuhusu ufafanuzi wa suala hili.⁣

#uchaguzi #marekani #upigajikura #mhamiaji #greencard #raia #ukaaziwakudumu #voa #voaswahili #sifa #kugombea #nafasiyaurais #sifa #wazazi #kuzaliwa