Ivanka azuru Ethiopia, Ivory Coast

Ivanka Trump, kushoto akutana na Rais wa Ethiopia Sahle-Work Zewde, kulia, katika Kasri ya Rais, Addis Ababa, Ethiopia on Monday Aprili 15, 2019.

Ivanka Trump, binti wa Rais Donald Trump na mshauri wake mkuu, anafanya ziara nchini Ethiopia ambapo Jumatatu amekutana mjini Addis Ababa na viongozi wa Kanisa la Kiorthodox la Tewahedo. katika ibada ya misa kwenye kanisa la Holy Trinity Cathedral.

Pia Ivanka anahudhuria kongamano la kiuchumi la wanawake barani Africa, siku ya Jumatatu wa kuwashirikisha na kuwahamasisha kiuchumi wanawake.

Katika kongomana hilo, atapata fursa ya kuzungumzia mradi wa dola millioni 50 ulioanzishwa na baba yake ili kuhamasisha ajira kwa wanawake katika nchi zinazoendelea kiuchumi.

Rais Donald Trump alitia saini hati ya rais ya usalama wa kitaifa mwezi Februari kutambua juhudi za maendeleo na mafanikio ya wanawake ulimwenguni-WGDP.

WGDP inaeleza ina matumaini ya kuwafikia wanawake milioni 50 ifikapo 2025 kupitia kazi za serikali ya Marekani na marafiki zake.

Kabla ya hapo Ivanka alitoa heshima kwa wahanga 157 waliopoteza maisha katika ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines mwezi uliopita.

Ivanka Trump amekutana pia na Rais wa Ethiopia Sahle Work Zewde na baadae atamtembelea Waziri Mkuu Abiy Ahmed kabla ya kuelekea Ivory Coast kushiriki kwenye mkutano unaozungumzia fursa za kiuchumi kwa wanawake wa kanda ya Afrika Magharibi.

Nchini Ethiopia tayari amekutana na wafanyakazi wanawake katika kiwanda cha kahawa na kutembelea kiwanda cha nguo kinachoongozwa na mwanamke.

Haikufahamika bado kama utata unaomkumba Rais wa Marekani utaibuka wakati wa ziara ya binti yake huko Afrika. Rais amekuwa na maneno makali kuhusu Afrika na wahamiaji wake.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.