Iran yakanusha madai ya Marekani kuhusu droni iliyoishambulia meli ya mafuta pwani ya India

Nasser Kanani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

Iran Jumatatu imekanusha madai ya Marekani kuwa droni moja iliyorushwa kutoka Iran iliilenga meli ya mafuta iliyo kuwa katika pwani ya India wiki iliyopita.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanani alijibu swali kuhusu tukio hilo kwa kusema madai ya Marekani yalikuwa “hayana msingi.”

Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilisema Jumamosi kuwa “droni iliyolenga kushambulia iliyorushwa kutoka Iran” iliipiga meli iliyokuwa na bendera ya Liberia, inayomilikiwa na Japan na kusimamiwa na kampuni ya Chem Pluto ya Uholanzi.

Tukio hilo lilisababisha moto mdogo katika meli ya mafuta hiyo, lakini ulizimwa mara moja na hapakuwa

Waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen wamelaumiwa kuhusika na mfululizo wa mashambulizi hivi karibuni dhidi ya meli kadhaa katika bahari ya

Sham baada ya kutahadharisha watashambulia meli zote wanazoziona kuwa zina mahusiano na Israel.

Jumamosi, shirika la habari la Tasnim la Iran limeripoti kuwa afisa mmoja wa Kikosi cha ulinzi Revolutionary Guard nchini humo alionya uwezekano wa kulazimika kufunga njia kadhaa nyingine za majini iwapo vita vitaendelea huko Gaza.

Baadhi ya taarifa katika habari hii zinatokana na mashirika ya habari ya AFP na Reuters.