Afisa wa ujasusi wa Israel alinyongwa Jumamosi nchini Iran, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ya Iran (IRNA).
Inadaiwa kuwa mtu huyo alituhumiwa kuiba siri na kuzikabidhi kwa Mossad, shirika la ujasusi la Israel, IRNA imesema. “Mtu huyu aliwasiliana na idara za kigeni, hasa Mossad, akikusanya taarifa za siri, na kwa kushirikiana na washirika, alitoa nyaraka hizo kwa idara za kigeni, ikiwa ni pamoja na Mossad”, IRNA ilisema.
Mauaji hayo yalifanyika huko Zahedan, mji mkuu wa mkoa wa kusini mashariki mwa Iran katika jimbo la Sistan na Baluchistan. Ilisema kuwa mtuhumiwa alikabidhi taarifa za siri kwa “afisa wa Mossad” kwa lengo la “propaganda kwa makundi na mashirika yanayoipinga Jamhuri ya Kiislamu”.
Haikusema ni wapi madai hayo ya makabidhiano yalifanyika. Haikufahamika ni lini mtu huyo alikamatwa, lakini IRNA ilisema rufaa ilikataliwa.
Forum