Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 23:04

Iran inaondoa masharti ya Visa kwa nchi 33 ikiwemo mataifa ya Ghuba


Ramani ya Iran pamoja na nchi zinazopakana nazo.
Ramani ya Iran pamoja na nchi zinazopakana nazo.

“Wizara ya utalii inaamini kuwa sera yake ya kufungua mlango huu itaonyesha dhamira ya Iran ya kushirikiana na nchi mbalimbali duniani”, ISNA iliripoti.

Iran imesema inaondoa masharti ya viza kwa nchi 33 ikiwemo mataifa ya Ghuba kama vile Saudi Arabia ambayo Tehran imekuwa na uhusiano baridi kwa miaka kadhaa hadi makubaliano ya hivi karibuni, shirika la habari la Iranian Students News Agency (ISNA) limesema Alhamisi.

“Wizara ya utalii inaamini kuwa sera yake ya kufungua mlango huu itaonyesha dhamira ya Iran ya kushirikiana na nchi mbalimbali duniani”, ISNA iliripoti.

Uamuzi huo utaongeza idadi ya nchi au maeneo hadi 45 ambayo raia wake wanaweza kutembelea Iran bila kuhitaji kupata visa, ilisema. Hatua hiyo ni hatua nyingine ya kuimarisha uhusiano kati ya Iran na Saudi Arabia hasa baada ya miaka kadhaa ya mvutano kati ya mahasimu hao wawili wa Ghuba wanaozalisha mafuta.

Riyadh na Tehran zimeungana na pande zinazohasimiana; Syria, Iraq na Yemen katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Mashambulizi dhidi ya miundombinu ya mafuta ya Saudi Arabia ambayo maafisa wa Magharibi wanailaumu Iran na vikosi vyake vya kibaraka wa Kiarabu, vilitishia katika miaka ya hivi karibuni kuipeleka Mashariki ya Kati katika mzozo zaidi. Iran imekanusha kuhusika na mashambulizi hayo.

Forum

XS
SM
MD
LG