Wanaharakati raia wa Marekani wenye asili ya Iran wanaotaka kuwaondoa maafisa wa zamani wa Iran kutoka katika chuo cha Marekani ili kuwawajibisha kwa rekodi mbaya ya haki za binadamu kwa Jamhuri ya Kiislamu wanasema chuo cha Marekani kilichomsimamisha kazi afisa mmoja wa zamani mwezi uliopita kinahitaji kufanya mengi zaidi.
Alliance Against Islamic Regime of Iran Apologists (AAIRIA) pia unaiambia VOA kwamba kusimamishwa kwa Mohammad Jafar Mahallati katika Chuo cha Oberlin cha Ohio kumelihamasisha kundi hilo lisilo la kiserikali kumlenga afisa wa pili wa zamani wa Iran kwa kuondolewa katika taasisi nyingine ya elimu ya juu nchini Marekani.
Chuo cha Oberlin kiliviambia vyombo vya habari vya Marekani mapema mwezi huu, kwamba kilimweka Mahallati katika likizo ya utawala isiyo na kikomo hapo Novemba 28. Haikutoa sababu ya hatua hiyo.
Mahallati alihudumu kama balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka 1987 hadi 1989. Kisha aliondoka katika serikali ya Iran kwa ajili ya kufundisha na kufanya utafiti katika vyuo vikuu kadhaa vya Marekani na Canada, ikiwemo na Chuo Kikuu cha Columbia cha New York katika miaka ya 1990, kabla ya kujiunga na chuo cha Oberlin kama profesa wa dini mwaka 2007.
Forum