Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 04:07

Iran yaonya kusitisha safari za meli za Meditteranean kutokana na vita vya Gaza


Picha ya meli ya mizigo kwenye bahari ya Mediterranean.
Picha ya meli ya mizigo kwenye bahari ya Mediterranean.

Kamanda mmoja wa kijeshi wa Iran amesema kwamba bahari ya Mediterranean huenda ikafungwa iwapo Marekani na washirika wake wataendelea kutekeleza ukatili huko Gaza, bila kueleleza namna hilo litakavyofanywa, chombo cha habari cha serikai ya Iran kimesema  Jumamosi.

Iran inaunga mkono wanamgambo wa Hamas dhidi ya Israel, wakati ikilaumu Marekani kwa kile imetaja kuwa uhalifu wa kivita huko Gaza, ambako makombora yaliorushwa kwa wiki kadhaa yameua maelfu ya watu na kusababisha maelfu wengine kutoroka makwao.

“Hivi karibuni watashuhudia kufungwa kwa bahari ya Mediterranean, kwenye njia ya Gibraltar pamoja na nyinginezo,” Chombo cha habari cha Tasnim, kimemnkuu Jenerali Mohammad Reza Naqdi, ambaye ni mratibu wa jeshi la kitaifa la Iran.

Kundi la Houthi linaloungwa mkono na Iran, ndani ya mwezi mmoja uliyopita limekuwa likishambulia meli za mizigo kwenye bahari ya Shamu, kama majibu kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza, na kupelekea baadhi ya makampuni ya meli kubadili safari zao.

Ikulu ya Marekani Ijumaa ilidai kuwa Iran inahusika pakubwa katika kupanga operesheni dhidi ya meli za mizigo kwenye bahari ya Shamu.

Forum

XS
SM
MD
LG