Siku ya Jumatatu taifa hilo la Asia Kusini limeripoti kesi 368,147 katika saa 24 zilizopita.
Wakati India ina moja ya makampuni makubwa ya kutengeneza chanjo duniani, Serum Institute of India, asilimia 2 pekee ya watu billioni 1.3 ndio wamekwisha pewa chanjo, kwa mujibu wa ripoti za ndani.
Mkuu wa utawala kwenye ofisi ya Rais Joe Biden, Ron Klain ameiambia televisheni ya CBS Marekani imeanza kupeleka msaada India.
Hata hivyo, Marekani pia imechukua hatua za kuzuia kusambaa kwa virusi. Kuanzia Jumanne, hakuna ndege zitaingia Marekani kutoka India.
Marekani ilipeleka nchini India vifaa tofauti vya kupambana na janga la COVID-19, ikiwemo mitungi ya oxygen, barakoa na vifaa vya kufanya vipimo vya COVID-19 kwa haraka. Nchi kadhaa za dunia pia zilituma msaada nchini India.