Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 05:25

India yarekodi maambukizi zaidi ya laki moja ya COVID-19


Watu wakisubiri kupanda mabasi mida ya msongamano wa usafiri katika kituo cha basi, wakati taifa hilo likishuhudua kuenea kwa COVID-19, huko Mumbai, India April 5, 2021. REUTERS/Niharika Kulkarni
Watu wakisubiri kupanda mabasi mida ya msongamano wa usafiri katika kituo cha basi, wakati taifa hilo likishuhudua kuenea kwa COVID-19, huko Mumbai, India April 5, 2021. REUTERS/Niharika Kulkarni

Wizara ya Afya ya India inasema Jumatatu imerekodi kesi mpya 103,558 ikiwa ni viwango vya juu ya virusi vya Corona, idadi kubwa kwa siku 2020 huko katika taifa hilo la Asia Kusini.

Mumbai, mji mkuu wa kibiashara wa India, na mji mkuu wa jimbo la Maharashtra, hivi sasa uko chini ya masharti makali yanayowataka watu kusitisha biashara na kubaki nyumbani.

Karibu nusu ya kesi mpya za virusi vipya nchini humo zimerekodiwa Maharashtra.

Nawab Malik, waziri katika serikali ya jimbo hilo akizungumza na waandishi wa habari alitangaza amri ya kutotoka nje wakati wa usiku kuanzia saa mbili usiku hadi saa moja asubuhi kwa saa za huko kuanzia Jumatatu.

Vituo vya biashara vyenye maduka mengi maarufu Malls, sinema, baa, mahoteli na sehemu za ibada zitafungwa kuanzia Jumatatu jioni.

Masharti kamili ya watu kutotoka ndani iwapo huna shughuli maalumu ya kufanya yataanza wikiendi.

Ni mataifa mawili pekee ndio yamethibitisha kuwa na kesi nyingi mbali ya India, ambapo kwa wakati huu ina zaidi ya maambukizi milioni 1.2, kulingana na chuo kikuu cha John Hopkins cha Marekani, kituo kinachofuatilia kesi za virusi vya Corona. Marekani ina kesi milioni 30.7, wakati Brazil inakaribia maambukizi milioni 13.

XS
SM
MD
LG