Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 06:02

India yakumbwa na wimbi la pili la maambukizi ya Covid 19


Kesi za Covid 19 zaongezeka kwa kasi India.
Kesi za Covid 19 zaongezeka kwa kasi India.

India iliripoti maambukizi mapya zaidi ya laki 3 ya COVID-19 siku ya Alhamisi, ikiwa ni idadi kubwa sana kwa siku moja kuliko taifa lolote lile wakati wa janga hili la Ulimwengu la mwaka mzima.

Ikilinganishwa na Marekani kwa upande mwingine, ambayo iliandikisha idadi kubwa ya wagonjwa katika siku moja zaidi ya laki 3 tarehe mbili Januari kulingana na Kituo cha taarifa za corona cha Johns Hopkins.

India, nchi ya pili kwa idadi ya watu duniani, inapambana na wimbi la pili la maambukizi ya corona ambayo yamesukuma mfumo wa huduma za afya ya nchi hiyo ukiwa katika hatari ya kuanguka.

Hospitali ziko karibu kujaa na zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa mitungi ya oksijeni. Uhaba wa oksijeni ni mkubwa sana kiasi kwamba mahakama kuu katika mji mkuu, New Delhi, iliamuru serikali ya kitaifa ibadilishe oksijeni kutoka kwenye matumizi ya viwandani kwenda hospitalini.

“Omba, kopa au uibe”, majaji walisema kujibu ombi la hospitali ya New Delhi.

Alhamisi ni siku ya nane mfululizo ambapo India imeandikisha zaidi ya kesi mpya laki 2 za corona, ikisukuma idadi ya jumla ya maambukizi kwa zaidi ya milioni 15.9, ikiwa ni ya pili nyuma ya milioni 31.8 nchini Marekani.

XS
SM
MD
LG